Serikali, WFP, UNCDF kuwezesha 80% ya watanzania kutumia Nishati Safi ya Kupikia

Na Zuwena Msuya Dodoma Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (WFP), Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) na wadau wengine wa maendeleo ndani na nje ya nchi wanafanya jitihada mbalimbali ili kuwezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ndani ya kipindi cha miaka kumi